1 Corinthians 10:7-12

7 aMsiwe waabudu sanamu, kama baadhi yao walivyokuwa, kama ilivyoandikwa, “Watu waliketi chini kula na kunywa, kisha wakainuka kucheza na kufanya sherehe za kipagani.” 8 bWala tusifanye uzinzi kama baadhi yao walivyofanya, wakafa watu 23,000 kwa siku moja. 9 cWala tusimjaribu Al-Masihi, kama baadhi yao walivyofanya, wakafa kwa kuumwa na nyoka. 10 dMsinung’unike kama baadhi yao walivyofanya, wakaangamizwa na mharabu.

11 eMambo haya yote yaliwapata wao ili yawe mifano kwa wengine, nayo yaliandikwa ili yatuonye sisi ambao mwisho wa nyakati umetufikia. 12 fHivyo, yeye ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke.
Copyright information for SwhKC